Kijana Wa Cyber

“Yes customer, karibu sana. Nikusaidie aje?” my famous phrase pale kwa cyber. Mimi huwa na a good customer care service. Sifa zangu zimeenea saana. Ndio maana cyber nyingi za Nakuru hunitafuta wapate services zangu, but I turn down their offer. Mishahara yao midogo midogo, daaah! 😂😂

Kama kawaida kwa biashara kuna siku utapata customers wengi sana, sales ikuwe nyingi. Kuna siku utapata customers kiasi sales ikuwe chini. Pia kuna siku inawezekana usipate customers at all (though si rahisi). All in all usianze kujichukia juu ya hizi siku mbili nimetaja. Kumbuka ile siku ulimake sales nyingi venye ulishukuru Mungu sana. Hivo hivo siku hautapata mapato mengi usilaumu Maulana. Huwa nasema Ukipata Shukuru, Ukikosa Usikufuru

Ilikuwa July, 2019. Jumapili moja. Customers walijaa wakihitaji cyber services. So nikawahudumia mmoja kwa mwengine; wamama kwa wazee, wakubwa kwa wadogo na hata vijana pia. Kidogo tu hivi, masaa kumi hapo, kidosho fulani akaingia…

“Habari yako, naomba kuhudumiwa, unaweza sahi ama uko busy sana?” aliniuliza. Nikamjibu “yes, naweza kukuhudumia, mwanzo utangoja nimalizie hawa customers kwanza. Na pia naona net yangu iko slow leo.” Akasema atachelewa na ametumwa sokoni sasa angerudi kesho yake baada ya kutoka chuo. Mimi nikajua tu promises are just words. Though alikuwa mremboo😍 na atarudi kweli? Acha tungojee kesho.

“Sasaa, nimerudi, I hope net leo iko poa” ni yule yule. Mimi kimoyomoyo nikajiambia “kumbe alikuwa serious, aaah, hapa siharibu hii chance, huyu lazima tu nimkatie. Sijui nimwambie nishampenda”
My mouth “eeh, net iko poa sana, oooh naona umerudi, kumbe wewe si mwongo” 😅😅
Saa hizo tu nikamalizia customer nilikuwa nahudumia haraka tena sana. Nikafungua mlango ya counter. “Ingia mrembo, keti kwa hii stool nikumalizie haraka. Hapana nitakufanyia polepole yaani taratibu, mpaka ufurahie, alafu urudi tena nikufanyie” Dem aka-smile😁 nikajua baas huyu anaweza vumilia jokes zangu. Nilikuwa napima boundaries mwanzo. Akaingia akaketi alafu nikafunga hiyo mlango.

“Nataka unifungulie Google Account” alisema. Mimi nilidhani amekuja akitaka service kubwa kama KRA pin, lakini kwa biashara tunasema, hela ni hela, hizo coins ndizo zinajenga noti. Yaani haba na haba hujaza kibaba. Kumbukeni kufungua hiyo Account ni dakika kama tatu pekee. Hiyo hauwezi nitosha kuwasilisha ujumbe wangu, hapana😂😂 Nitakuwa mjanja.

“Sasa nitahitaji majina yako kamili, ID number, Date of Birth na nambari ya simu” nilimwambia. “aaai, hizo details zooote, namba si lazima, ni hivi nyinyi vijana wa cyber mnakuaga, mnakusanya namba za wasichana ovyoovyo”

Huyu atawacha nifanye kazi yangu ama atanifundisha!!!

“…kuna code imetumwa kwa simu yako, nisomeee… tutatumia namba yako kama password yako ndo usisahau…” nilikuwa namwambia. Si niliwaambia hapo juu nitakuwa mjanja😂💪🏾 alisema namba, hadi sasa nika-cram. Nikamaliza akasema anataka kuenda nyumbani sasa. “Sasa ju ni 30 bob na umenikaisha sana, kata 10 nikupee 20 bob” mschana ana-burgain? Huyu nitawezana? Kama wewe ni mwanabiashara, kuna vitu viwili haviendani: Mapenzi na Biashara. Usichanganye hizo vitu. Mimi alinilipa zangu 30 bob😂😂 akatoka akisema “Asante sana Mc Raj, barikiwa sana, byee” akatoka aki-smile😁

Hapa sasa roho ilifurahia saana😅 Mbona hakuja asubuhi anijengee siku mapema? Lakini ni sawa, siku itakamilika vizuri. Saa mbili usiku ilifika, nikafunga biashara kama kawaida.

Wasomaji, ni saa tano za usiku, hii masaa kuna upweke fulani inakutandika, mnanielewa, sio?😂😂 Nikaamua sasa kutumia akili, kwa akili nikapata namba ya yule customer iko bado. Nikafika Whatsapp nikatuma message; “0798….40 ndiyo itakuwa password yako ndiyo usisahau😅” apa I was expecting blueticks nikikumbuka aliniambia kazi ni kukusanya namba za waschana ovyoovyo.

Muda si muda, punde si punde, naskia message, nikafungua mbio mbio kuangalia nasoma “bro niokolee Mia mbili nitakurudishia kesho ikiwa Mia tano” niliudhika😬huyu hajui nilikuwa nangojea good news, yenye ingebadilisha title yangu itoke kwa Single boy. Nili-reply “Bro ngojea hiyo kesho ndo upate hiyo Mia tano.” Dakika kama tatu napata message tena. This time isikuwe Brayo tena na shida zake. Kufungua nikasoma “heey😅nilijua tu ungenitext, design ulirudia rudia namba yangu, najua ni wewe Raj, mamboo” Hapa sasa ndo nilitamani ku🎶tuma kitu, tuma kitu, nitume pia na ya kutoa🎶. Yaani msupuu akuje tu kejani saa hiyo hiyo, ju naona bet ilikuwa imeivaa🤲🏾💯😂

Wambui alikuwa mwanafunzi wa Mwangaza College, akisomea Interior Design. Nikaanza ku-imagine venye atarembesha nyumba yetu😍 venye ata-design mavazi yetu tutese watu huku nje. Hahaha!! Just one reply can change your moods from zero to a hero. Yaani ni kama nilikuwa nimeshinda Lotto.

“Nikitokea shulee me hupitia apo kwa cyber nikienda home, nitakuwa nakuja kukusalimia siku moja moja ndio usiboeke na mimi” alinijibu after a long conversation between us. There was hope💯 There will be hope when she actually visits as she had promised. Tulizidi kuongea na Wambui, tukajuana vyema, Nilimpenda kusema kweli.

Friday sasa akitokea chuo akapitia kunisalimia. Alikuja akapata niko na customers wengi sasa nilikuwa busy. Ushawahi tamani kuambia customers waende warudi kesho🤣 Lakini nikakumbuka hatutakula mapenzi, nikamwambia atembee Jumapili ningekuwa free.

Wambui wangu alikuja Jumapili?? Hahaha!!!

Follow me on:
FB: Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc
Email: rajthemc55@gmail.com

LOVE or LUST (Episode 2)

… conversation was all good. Relationship ilikuwa strong sana, sijui ni kwa sababu ilikuwa mpya, nimesema sijui.
Niliona nmemkamata Fiona, smati wangu. Sasa alikuwa wangu. Hakuna kitu nzuri kama kupenda anayekupenda,kumtunza kumlinda na kumpa anachotaka bora kiwe kwa uwezo wako. Tulikuwa tunakutana mara kwa mara, tufanye mambo mawili matatu kama kusoma Biblia!! Ona unanishuku juu huwa husomi Biblia.

Fiona was the type of woman I wanted. I got her. Glory be to God.

After Long Holiday si nikarudi chuo, Kakamega. Yeye alikuwa anasomea Nakuru. Hapa sasa nika-sign deal ya “long-distance relationship” kitu ngumu sana kwa maisha yangu. Nikakumbuka msemo; Tunza huyo uko naye, kurukaruka haisaidii.

Tulikuwa tunaongea kwa simu mara kwa mara, kuhakikisha mapenzi yetu iwe dhabiti. “Lakini sasa, miezi nne zote tukiongea tu kwa simu, ni ngumu sana, Babe” aliniambia. Alaa!!!

Miezi mbili hivi ikapita, mawasiliano yakaanza kuwa fupi, anajibu anavyotaka, wakati anataka. Inauma. Narudia tena. Inauma.

Ushawahi pewa Storo bonus 10:56 p.m na zinaisha 12:00 a.m? Unaelewa chenye nasema hapa. Nikapitia “contact list” yangu, kuona watu naweza pigia simu. Kumbuka, You don’t just call anyone past 10 pm unless you two are so connected. Out of 716 contacts, napata wasichana watatu naweza pigia simu. Bahati mbaya wawili wakawa mteja,hawapatikani!

Mimi huyoo, nikampigia Fiona, tuongee kwa dakika hamsini kwa sababu ilipita muda mrefu bila sisi kuongea.

Nilipiga simu akashika.
“Heeeey, sasaa smatiii” nilisema. Enyewe alikuwa mwanamke smart, chocolate color, nywele laini,nguo za kung’ara latest designs alafu kuongezea sasa, alikuwa mine.

“Ni nani kwanza?” Aliniuliza. Waaah!!!! Mrembo wangu ananiuliza mimi ni nani? Apo nikakumbuka akiniambia hawezani kuongea na mtu yuko mbali. Maybe she lost interest in this long distance relationship. Maybe.

“Ni Raaaaaaaaj”
“ooh, ebu kata simu kwanza”
“You mean I hung up?”
“eeh, kata simu wewe, husikii”
Si angesema ata nikatie simu anipigie.
Msinicheke, leo mimi kesho wewe.

Hadi leo sijawahi pigiwa simu, ata message sijawahi pata. I was right, She definitely lost interest in this long distance relationship. “Alipata chenye alikuwa anataka akaniwacha”

Women play too. Kuna wasichana wajuaji siku hizi. Nilitumiwa na nikawachwa.

Anyway, I moved on.

Know your position in someone’s life. Usishinde umekasirika

FB: Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc

Email: rajthemc55@gmail.com

LOVE or LUST (Episode 1)

Ilikuwa 2019 December, nmeenda pale Town na pesa zangu chache, along the streets nikakutana na Dem fulani mrembo🌹😍 siku hizi wanaitwa “Mali Safi.” Alikuwa medium height, chocolate color pia alikuwa amezibeba utadhani ako gangari. Alikuwa Mama la Mama, yaaani: “🎵…chocolate color, nywele laini, lips mafuta na zinashine. Nguo za kung’ara, your design👌🏽…🎵” imebaki hiyo part ya “Thanks To The Lord Now You Are Mine” ju bado hakuwa wangu😂.

Tukitembea macho yetu yakakutana, nikajua baas, she’s the one💯. Ndio nikakumbuka huku si kwa wazungu eti kuna Love at the first sight. Halafu kawaida ya huku Kenya ukisalimia msichana atadhani unamtaka. Ndio, ni ukweli unamtaka lakini haifai afikirie hivyo😅. Tukapitana nikaelekea zangu. Baada ya shughuli nikaenda pale kwa stage kuabiri matatu ya kunifikisha nyumbani. Kama kawaida mimi hupanda zile gari za kusonga, sio zile za pale stage. Nilichanuliwa. Kuna wakati rafiki yangu Njuguna aliniona nimeketi kwa matatu apo Main stage nangojea ijae, alishout “wee Mc Raj, wacha kupanda matatu kwa stage kama wamama wa soko, tuabiri matatu za kusonga, kuwa mjanja kaka.” Nilishikwa na aibu sababu kila mtu aliniangalia. Toka hiyo siku nilikuwa mjanja😂😂.

Bado hamjasahau yule mrembo wangu. Aaah, sikia nimeanza kumuita wangu. Baada ya kuingia kwa hiyo matatu, huyo msichana pia akaja akaingia. Yeye pia alikuwa mjanja😅Aliniona na akaketi kando yangu kwa sababu kulikuwa na nafasi. Nadia Mukami aliimba Kazi ya Mungu haina makosa.

Sasa ilikuwa wakati wangu wa kuonyesha ushujaa. Kijasho chembamba kilinitoka. Wanaume mnanielewa nikisema hivi. Nikakumbuka msemo; bahati haibishi mara mbili. Nikamsalimia “mambo” halafu nikarudi kwa simu yangu kuendelea kuandika #StoryZaMcRaj. Sikutarajia jibu toka kwake. Nikaskia “poa saaaaaaana” I hope mumegundua hizo “a” kwa neno sana. This means she was very interested in the conversation.

Hadithi fupi huwa sikosi, ukiwa na mimi hauwezi boeka. Si eti najigamba😂. Niruhusu nimuite “smatii” ju kusema kweli alikuwa smart❤️ Akaniambia anashukia Pondamali. Hapo nikajua ni msichana wa ghetto. Hawa wasichana huwa na moyo mzuri na wa upendo. Ukifanikiwa kupata mmoja mtunze, atakutunza pia. Mimi nilikuwa nashukia Langalanga, kabla ufike Pondamali.

Tuliendelea na stories, hakuwa wale wasichana boring wenye ukisalimia “mambo” atajibu “poa” alafu angoje uulize maswali yeye akijibu. Kama wewe ni hii type ebu rekebisha tabia tafadhali😂. “kwani naenda nyumbani kupika??” nilijiuliza. Na ni ukweli ilikuwa zamu yangu ya kupika. Lakini sasa nikishuka mwanzo niwache huyu mrembo! …

Most of these beautiful ladies are already taken; in most cases *Taken for granted*😉 Ndugu yangu, usiogope ku-approach msichana kama amekufurahisha.

Huyu msichana alipiga stories hadi nikatamani nisimamishe gari kwanza tuingie hotelini tule mawili matatu ndio tuendelee na safari. Nilimlipia fare, Ksh 30. Kumaanisha hiyo jioni yule Kamau wa mturaa hangepata pesa yangu. Ksh 30 si nyingi, kuliko utumie msichana fare ya Ksh 1500 na akule yote. Mimi siwezi tuma, wewe kuja na yako nitakurudishia😂.

“By the way Raj, what’s your plan in this life?” Aliniuliza. Si wasichana wote wanaweza kuuliza kuhusu life goals. Mimi nishaanza kupenda huyu msichana. Huu ndio wakati mwanaume huanza kudanganya. Mimi nilijiambia nitasema ukweli. Nilimwambia nataka kuwa “Financially Independent” huwa nafanya biashara ndogondogo pale kwenye chuo kama kuuza nguo na lollipops. Smatii aliniangalia kwa macho nikajua nimejidunisha. Msichana mrembo kama yule hangevumilia mwanaume anayeuza lollipops.

“Like seriously, all that struggle ndio upate pesa. I really appreciate that. Si kila mwanaume anaweza tembea door to door akiuza products zake, yahitaji bidii na courage. Get a hug Raj” Sikuamini chenye nilisikia. Nkamsongea nikapata hug. Nilifurahia sana😁😁.

Joto ilizidi kwenye gari, nikatoa jacket. Nilikuwa nimevalia T-shirt ilikuwa na logo yangu; MC RAJ. Smatii aliiona akaniuliza “Are you also an Mcee?… Your girlfriend must be very lucky, a grinder and a lover all in one package but she also has a huge task, to support you morally, psychologically and even financially” Mkieza jua ata sikuwa na girlfriend😂 Hii hukuwa tactic wasichana hutumia kujua kama uko na mpenzi😆. Nikamjibu “yeah, she is a very supportive lady” Niliona sura yake ikibadilisha, furaha ikapotea.

Nikaendelea, “when you have life goals, you don’t just date any girl you come across, you have to look for a lady with vision as well. Sijawahi pata Dem wa hizi qualities. I wish nipate dem kama wewe.” That was me shooting my shot👌🏽😂✔️

Nilizoea kukataliwa, sasa hata huyu akinikataa hatakuwa wa kwanza, nilijisemea hivyo kimoyomoyo. Before anipee jibu tukasikia “Oyaa joomba apo nyuma na mnyonyoo wako, gari imefika mwisho, tushuke.” Kumbe tulipiga stories mpaka tukapitishwa makwetu. Nikajisemea “Mungu, si hii safari ingekuwa ya toka Nakuru hadi Kakamega” lakini nikakumbuka ningemlipia fare ya Ksh 1,000.Elfu mbili ingetoka wapi? Nikajisemea “Mungu wacha tu, Asante” 😂😂. Tulitembea sasa kurudi Pondamali. Alinipa namba zake za simu. … To be continued … Email: rajthemc55@gmail.com FB: Mc Raj Twitter/IG: @rajthemc

Green lights…”Stupid” Mc Raj

#StoryZaMcRaj

Most of us tunakuaga na wale uncles wenye roho safi, ukiomba dooh amekuskumia👏🏾👏🏾 any help anakusaidia bila questions. Alafu sasa kuna wale rich stingy uncles, hao wajipigie story zao✋🏾😂😂😂 So kuna huyu uncle yangu alipewa transfer hadi Kakamega toka Busia. The last time nilikuwa kwake Busia, life ilkuwa fity, saa kumi apo tungeendea mbuzi choma palee, alafu na Tusker ati nisikuwe mlevi😆 ye akatandika makali. Ni ule uncle mwenye pesa zake ni za starehe tu💯💯 in future I want to be that uncle 🙏🏾😂😂
So ju tumezoeana nikam-text…

…”Niaje uncle, si u-organize nikamu nijue place unaishi… ni kitambo sana manzee”
ye haezi nipiga blueticks😂 akajibu “aah, hiyo ni idea fity, kamu hivi on Saturday, naishi huku side za Sigalagala. But I’ll link you na jamaa flani unichukulie documents fulani pale Kakamega town ukuje nazo”
Na akatuma hadi ferari, plus ya kukula kwa roady. asante Jehovah🤲🏾 that was on Thursday. ju zile dooh zilikuwa kibao, si nkaskumia mamaa credo ya 100, asione chali yake hukua amesota saaana😆😆
Kumbuka hii ni ile wiki ya kwanza yenye president Kenyatta…

…alitangaza curfew🚔Sato ilifika, nikatravel kuishia, but nilitoka masaa tisa. After 2 hours of traveling, matatu ikapata puncture. That was 5pm😢😢 took them 50 minutes kuunda,ndo tukaendelea na safari🙏🏾 but according to the time, singefika hadi Sigalagala hiyo jioni. Na sikuwa nimebeba funguo za mansion😅 yangu pale chuo. Na ata ningekuwa nazo singeenda kwangu, Landlord angedai rent😂😂kuna huyu morio wangu, Lorcents Photography alikuwa within Katch, nikam-text “oyaaa Lorcents, manzee nnatravel kuja Katch na ntafika late, na kuna curfew, ka unaeza ni host niendelee na safari kesho” akaniambia “iza manzee, nilitravel kiasi siko kejani, but acha nikulink na cousin yangu a kuhost leo usiku”…

…”walai shukran G👊🏾, apo itakuwa shwari sana manzee” walai usiwahi underrate friendship za high-school, huyu morio tulisoma chuo moja, ona venye si huokoleana🙌🏾
Within kitu daika 20 hivi napigiwa simu “heeey sasaa, nimeambiwa na cousin yangu uko stranded, that I should host you for the night” wasee kumbe cousin yake alikuwa dem😍😍alafu sauti supuu, weuuh😁 nikajibu kwa English pia😂 “yeah maan, I’m almost kufika town”… Ndo nakumbuka leo nilisema yeah man🤣🤣 shida ya kucram vitu🚮😂 “okay, ukishuka tao, ju itakuwa almost 7 siezi fika huko, chukua pikipiki ikufikishe Joyland, hapo ndo naishi, then unicall nikukujie kwa junction” apo ndo ile…

…unaskiaga furaha hadi ndani ya roho😅 Lorcents Photography apo ulikacheza safii bazeeng🙌🏾 hapa ndo nasemaga “morio mtrue”… nilishuka tao, nikachukua piki hadi Joyland, nikamcall akanikujia. Dem si alikuwa amebeba🤤🤤🙌🏾 alikuwa amebeba mchele na nyama yenye atapika supper🤣. Alikuwa chocolate color🙎🏽‍♀️, height ka yangu, aah acha tu niseme alikuwa size yangu😂mali safi yaani💯 tukafika kwake “Naitwa Joan, nmeambiwa unaitwa Raj… welcome to my ka small house, I guess it will serve you well, vumilia tu kwa leo” huyu dem hayuko serious, nyumba kubwa One-bedroom alafu anasema ka small house☹ “…alafu Lorcents ameniambia vitu most kukuhusu…boy m-humble… mlisoma pamoja…caring, funny…” …

…shukran tena G🙏🏾👊🏾 kijana alinimwagia sifa kadhaa kwa ule msupuu. So ni through pass nilikuwa napewa, ni mimi ilkuwa nisilalishe😂😂 story nyinginyingi, kujuana,… akapika wali nyama. Hiyo food ilkuwa taaamu🤤 she’s a wife✅ after hapo akaingia kuoga, pia me nkaishia kuoga. Akanipea t-shirt yake nilale nayo. Ushai treatiwa vifity🙌🏾 hadi unatamani uishi tu hapo😂 nikasahau nafaa niendelee na safari the following day. Ni dem anapenda hepi, akaseti movie, kumbuka tuko kwa bedroom yake. Mungu ni mzuri🙏🏾 hakuwa na mattress mbili, ju ningelala kwa floor ya sitting room😆 tukawatch movies kwa laptop. Ujue saizo me naficha kwanza😂 akachoka kuwatch, akaishia kuvaa night dress tulale😉 dem alivaa nguo…

…nguo flani hivi transparent👀 hapa nkajua leo nalishwa mbaaaya😀 after hapo akaniambia tuombe kwanza. Hizi ni gani sasa😉 anyway, she’s a prayerful lady, she’s still a wife✅🤣 after kuomba,for once akakunja sura, akakuwa serious akaniambia “na ujue me nimeokoka, ka ni kulala ni kulala, staki kusumbuliwa usiku” heartbreak💔alafu akaeka pillow katikati yetu. Ile design seizi mkaribia💔inauma bana, inauma😞 alafu ka ningesumbua aamue kunitupa nje, nje kuna mapolisi🙌🏾😂😂 manzee usingizi ilisumbua, ilikuja 4 a.m😂 tukalala, tukaamka kitu 8a.m. Apo akaunda breko. Tukaoga, sa nikakuwa ready kuishia tao, ni-pick zile documents nikiendaga…

…akasema atanisindii hadi tao. Singekataa. Ilkuwa Sunday sasa, upepo most, alikuwa amevaa para… hiyo kofia ikapelekwa na upepo😂 nkaonyesha skills zangu za kuruka, nkairukia, nkaishikia kwa hewa💪🏾😂. Dem akaniambia “thank you😊 unajua kurukia kofia na huezi ruka pillow ukuje side yangu hiyo usiku yote?”
waaaah🙌🏾🙌🏾😔 hiyo statement bado tu hunisumbua hadi leo.

😂😂😂

Email: rajthemc55@gmail.com

FB: Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc

Relationships, may be good or harsh to you, depends on what you stand for👌🏽

#StoryZaMcRaj

Relationship ingekuwa inapeanwa certificates, walai ningekuwa na nyingi sahi😅
Kuna huyu mschana nilikuwa na-date 2017,Msichana amazing👸🏼 sana, alikuwa anaitwa Fatuma. Ushai tandikwa na mapenzi❤ hadi ukafikiria kukuwa muslim😂😂 she was caring, loving, supportive bla bla bla. Huyu mdem alikuwa anafanya job kule tao, me on the other hand nilikuwa nmetafuta hustle sikawahi pata, nkaamua kukaa tu😒 alikuaga anatoka job, dem ameniletea Sprite pale, makeki, sometimes fruits, credit alikuwa anatuma pia😋 then we’d sink into movies before…

…before nimsindikize aishie home😂😂😂 najua kenye ulikuwa unafikiria🚮😂 alafu wadau, hakuna kitu poa ka broke boy aangukie mdem anafanya kazi, alafu akukubali jinsi ulivyo, utamu tu😋😂😂but pia mimi nilikuwa nachangia kwa hiyo relationship. Nilikuwa nampea password ya Wi-Fi, treasure🔥🔥😂 life was moving on swiftly until siku alinikaishaga chini akaniambia “hey darling, I love you. I accept you, being broke is part of the game but sasa my dear, you are comfortably broke… find something to do, hakuna dem atavumilia mashida.”
apo ndo unaskiaga Sailors waliimba Kurugushu💔karagasha💔kuruku,kungkung💔🤣kidagaa kiliniozea🙌🏾😞😞 kitu iliniuma sana ni…

…ni ati hizo makeki na macredit zimenitoka😂😂 Waah, sa ningedu!!! But enyewe huyu dem alikuwa right✅ skuizi hakuna mschana atavumilia mashida. Nkaanza ku-figure out kitu ningefanya na life yangu. Nkaanza hustle pale chuo. Viatu mdogo mdogo, tunguo, mathwiti, cookies😂 na kadhalika. Alafu hakunaga kitu fity ka kuwa na pesa zako mwenyewe.soooo sweet😍😍 she was right. She changed my mindset, not to be comfortably broke🤣 madem mnasoma hii story, nyi ndo mnaeza change huyo msee una-date, remind him of his… aaah English nyinginyingi ya nini🚮😂😂 iko hivi, mkumbushe worth yake, acheze ka yeye apige hustle na u-msupport kwa hustle yake. Sistee usivumilie mashida✖️unless mmeoana..

… so si tupesa tukaanza kuingia, Rajabu ni naaaani, nkatafta pengting mwingine🤤🔥🔥 aaai, kwaaani😂😂😂 so nkaanza ku-date Wanjiku pale Naks bado tu. This time at least I’d provide this and that😂😂like the “man” I was💪🏾😅 it was my turn kutwanga mschana wa watu na suprises😁nimnyoroshe na mapenzi😁
Kuna hii time niliamua kumpeleka out. Mmeskia kenye nmesema kweeli? Niliamua. Haikuagi a must bytheway✋🏾😂😂😂Bro usilazimishwe. Tukaishia ile hoteli niliai waambia “Summerland Hotel” ka kawa nkampea chance ya ku-order food. Akachapa order, times 2…sa ile time waitress analeta food, bahati mbaya akanikanyaga kiatu. Sinaga mbayambaya mimi…

…waitress aka-apologize “aki pole, sikujua. Don’t tell the Manager, ntalose job yangu” si mnaona mbona stakagi kufanyia mtu kazi, ati ukikanyaga customer bahati mbaya unaeza futwa kazi.ufalaa hiyo✋🏾✋🏾 me nkasema “issokey, haina mambo, hii ni kitu kidogo tu” guess what,huyu mdem nimepeleka date akaanza kuteta aki-shout ni ka ni yeye alikanyagwa☹☹ ati🗣️ “mbona unakanyaga boy wangu…waitress wengine hamkuagi na heshima… stupid… toka hapa…” shyeeet, ushai feel ni ka mwisho wa dunia😥😥hiyo kelele yote bana na si ye amekanyagwa.I felt dissapointed sana.
Ukitaka kujua tabia ya mschana mnunulie chakula😂 apo na apo nkapasha huyo dem…

… “Wanjiku, haifai u-treat mtu hivo ata ka amekukosea, akisema pole msamehe. Respect kila mtu na kazi yake…”
Tukatoka hapo after kula. Mimi ata ukuwe mrembo aje na hauna heshima, hatuezi elewana✋🏾that’s a NO✖️ uki-disrespect waiters ama watchmen, urafiki yetu inadedi, ata ukue nani. These people are someone’s parents and they’re trying so hard to put food on their tables manzee. I had to break up💔 with the girl, barely 2 weeks. Si mnaona mbona sipitishagi wiki mbili mbili😂😂ukitaka kujua tabia ya mschana, mpee chakula. Through the date nilijua hakuwa na respect… This goes to my bros…

…usivumilie tabia mbovu za mschana ati ju ni mrembo.Ziii✋🏾it’s not always about the beauty, character matters a lot💯💯 Besides, msichoke ku-date,thats the only way you can tell a person’s behavior before you think of settling with him/her in marriage.Zidi kuwa-sample✅😂😂 Me huona headlines “Nyandarua man kills mother and son” ingine “Mwanamke achoma mume wake akiwa ndani ya gari” is it because they didn’t take time to know each other before getting into marriage??
my advice: FIND A GOOD CO-PARENT FOR YOUR KIDS.
If you continue behaving normally, these relationships will treat you abnormally😆🔥bless up👊🏾

Email: rajthemc55@gmail.com

FB : Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc

Highschool, we all don’t like the place but we do like the memories we made there😅😅

#StoryZaMcRaj
Most times me hutulia naanza kukumbuka memories za kitambo. Memories never fade💥 my highschool experience was the best🙌🏾 kule ndo mtu hujua ku-survive kwa hii life.
Nilikuwa na hawa marafiki wajuaji sana. Kuna wakati mmoja alichota githeri ndoo full usiku kule kichen😆aaaai, githeri !!!😂Ka kawaida kulikuwa prefects wasoro, walimseti next day. Ikakuwa apewe suspension. The good thing was that;Principal aliingilia na akasema asipewe suspension,ati hiyo ilikuwa njaa😂😂 so Principal aka-offer huyo kijana treat for 3 days kwa ofisi yake. Alikuwa anakula chakula…

…chakula Principal alikuwa anakula. From breakfast to supper, for 3 days, weeeuh😋😋Hiyo sa ndo huitwa kismart😅 after one month morio mwengine naye akatoa scandal ingine. Alienda kukamua ng’ombe kwa farm🤣 huyo naye alishikwa😆Alidhani angepewa treat ka ule mwengine akunywe chai ya walimu. Kijana alipewa 2 weeks suspension na akarudi na ng’ombe wa maziwa😂😂Tukiwa breaktime tunaona mtu na babake wakiingia shule na ng’ombe,kijana ameshika kamba, mzee ako nyuma na kiboko🤣🤣🔥Apa sasa ndo watu walijua they should not behave abnormally✋🏾😂
Alafu highschool ilikuaga maisha ingine tricky bila dooh💵, me hukua na business ideas. Nkaanzisha biashara ya…

…ya kuuza biscuits nikiwa na Hilla [now Lorcents Photography📸]. Tulikuwa tunainvest pocket money kubuy boxes za biscuits, yes, business was illegal, lakini hii Kenya uki-follow every rule utakufa maskini nani😉Plus tulikuwa tumejuana na wale mabazeng💪🏾wa shulee, wenye ata prefects waezi wafanyia chochote. Box moja ilikuwa 250, 72 sachets tukiuza tunapata 360…ksh 110 profit per box. Ile shule tulikuaga ballers mbaaaya💵😂😂 Me sku ya githeri nilikuwa na-serve napeana githeri kwa form 1 hukua na njaa😆nabaki na supu. Naitaftia mandazi ka nane hivi, ongeza avocado🥑chapanisha na pilau masala ama girlic, haya,teremsha na soda🙌🏾 apo unasahau shida zako zooote🚮😂😂closing tulikuwa na dooh za…

…kubuy trending clothes and shoes. Supra👟ndo viatu zilikuwa trending zile enzi🔥😂watoto wa Magoha najua hamrelate✋🏾😂life was so sweet, I was even thinking of expanding my business. Pesa ishai kuwa tamu hadi unasahau uko shule😂.
Term 2 nilianza kuuza credit sasa, za Safaricom. Definitely kila shule ilikuwa na wajanja wa simu, so I utilized that opportunity. Credit ya 10bob nilikuwa nauza ksh 15. Hii biz ilipick aje fity💯 alafu nilikuwa na sinklet flani ya Green [niliiva hadi first year😂nkaitupa time nilikutana na old friend tao nikiwa na dem, ka nmeivaa akaniambia “Rajo bado hujai tupa hii nguo, toka high school, unaaibisha huyu dem bana”]…

…so chuo yote nilijulikana [na wajanja pekee ofcos✋🏾😂] ati me ndo msee wa credit, nikabandikwa jina Safaricom ju ya hiyo sinklet😅😅biz ilishikisha sana.
Sasa penye shida ilitokea ni Form 4 term 3💔 ju nilikuwa najiona mjanja sa ata nikiingia shule na credit sikuwa nazificha mbali. Kumbe kuna prefect aliniseti manzee😩Opening day napata walimu kibao kwa gate:Deputy, Boarding master, Class teacher na kadhalika. Time nmeingia kwa gate hivi naskia boarding master akiambia wenzake “Ndouyo ashafika” alaa😂I wasn’t even the best student in school, why were they waiting for me!!! Kiasi nmeanza kupigwa search ka mwizi☹️ nkaambiwa nitoe wallet…

…hawakupata😂 manzee nilikuwa targeted hadi nkaambiwa nitoke kwa line kwanza😂😂😂 “Toa viatu na socks kijana” kuzubaa kidogo kofi ya kisogo🖐🏾😂”sa unanipigia nini?” kitu iliuma kabisaa ni ati form ones walikuwa apo wakiona. Respect nilijua imeisha🤣 Time natoa socks hivi, credit zikaanguka chini. Fifty fifty, za 20 na za 10. Credit za ksh 4,500…zote zikachukuliwa na boarding master😭😭hapa career yangu ilkuwa imededi😬 na nkajua ni suspension, na Babangu hukua atariii, weeeeuh💥🙌🏾 the good thing is that Pricipal alisema form 4 yeyote asirudishwe nyumbani,tukae shulee tu-prepare for KCSE. Nilikuwa pale tu kwa gate ka mshukiwa nikingoja kujibu mashtaka😀Kuna huyu teacher mmoja pale akashout…

…”Mr. Karani, si tugawane hizi credo haraka kabla walimu wengi hawajajaa” pesa zangu ndo zinaongelelewa apa ivi☹️☹️ pale kulikuwa na ule teacher tulimpea nickname – Sisulu… Boarding master akararua credit ya ten akapea Sisulu na akamwambia “Sisulu chukua hii ya ten itakutosha. Ata hauna bibi, hauna watoto sa ata utapigia nani simu” 🤣🤣🤣🔥🔥kila mtu pale alicheka, students, teachers na watchmen. Sio fair✋🏾😂😂me nkaambiwa niingie ndani ntaitwa baadae. Walai nilikuwa nmesota mbaaya, na ni day 1,no cash no shopping. Sku ya githeri ni mi nilikuwa naambia wasee wanichangie ndo nishibe😂😂enyewe tables turn😂na saizo siezi piga simu home💔niliamua sasa kucheza hii game…

…Kiss Komanda Promise😂😂 watu Starehe boys najua ham-relate😂 Hii game ilikuwa tricky, ka umesota unachagua comand, alafu mnaset prices. At least apo ningepata kafifty😅 so kuna hii mbogi ilikuaga inatulia pale school farm time ya games, kutegea Day scholers wapite😂Ilikuwa Sato, sku ya entertainment na nyama😋nkaamua kucheza game. Nkaambiwa ni-sneak nikatie one of the dayscholers nichukue namba, in return kila msee apo anipee nyama yake, ilkuwa watu ka 23,hizo ni pieces 23 za nyama, ukiunganisha zote inaunda mbuzi ndogo💪🏾😂😂 ju nilikuwa pabaya, hiyo day nilivaa sinklet ile ya green😅 nikasneak out nikaendea namba, ju huyo dem alikuwa form 4 na walikuwa wanaenda shule hadi sato…

…nilivuka nikaendeaga namba, jioni kila mtu akacoperate akanipea nyama, sema tajiri tena💪🏾😂piece moja ilikuwa 10 bob, unauzia watu wa Nairobi😂 nikauza kadhaa nikapata dooh ya…..

*To be continued😂

Email: rajthemc55@gmail.com

FB: Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc

A lady called Wairimu

#StoryZaMcRaj
Pale kidato tulikuwa tunaambiwa “someni kwa bidii, University utapata waschana warembo hadi ushindwe kuchagua. Wasichana watakuwa wanajileta tu, kazi yako itakuwa kuwa-sample…” Na enyewe time ya closing ukipita town unaona madem wa campus venye ni warembo, unaamua kusoma kwa bidii ndo ufike huko. Design wao hurembeka mtu hata haezi jua saa zingine huwa wanalala njaa!!!

September 2017 nikapata chance ya kujoin ” The University of Choice”. Nilichapa wiki mbili, waschana hawajileti, aaaai, those teachers lied to us.
Ju hawakuwa wanajileta, nkaamua kuwatafuta.

Kuna huyu msichana nilikuwa namuona sana akiwa pekee yake. To me, alikuwa anti-social. I had to gain the confidence of approaching her.

Friday evening nikampata pale student’s centre, amekaa pekee yake akinywa Delmonte akienjoy hiyo breeze hukuwa apo. Nikamwendea, nikaanzisha conversation “sasa… I never see you with friends,would you mind if I become one…” Dem kumbe alikuwa social, niliexpect akuwe wale wasichana wa attitudes. Alinipa namba yake, akaniambia jina lake, Wairimu. A very fine Kikuyu lady; her skin complexion, chocolate hivi, figure fire, alafu alikuwa amebeba, weeeuh…nadhani pia alikuwa amebebea models wa hiyo chuo ju hawanaga kitu. Honestly hizo haga ndo zilifanya nimpende ata zaidi.

Tukiwa talking stages, with time we became so comfortable with each other, we earned the title “Babe/Sweetheart…”
I texted “Babe uko room?” “Yes, niko,I can’t wait to see you today” she replied. Nikaoga vizuri, luku safi, nikateremka kuelekea Hall 1. Toka hostel yetu, Hall 3,hadi pale ilikuwa three-minute walk. Hii ndo ilikuwa mara ya pili sisi kukutana, let me call it official meeting. Kufika pale nje ya mlango nikajiunda vizuri tena, wanaume mnanielewa apa. Nikabisha nkaambiwa niingie. Wairimu hakuwa, nkaambiwa na roommates wake ati ameenda nje kidogo kuanika nguo. Weeeuh, hawa roommates si walikuwa wameiva pia, ni kama waliambiana waishi kwa hiyo room. Within 2 minutes akakuja, I saw the beautiful smile on her face, I saw love. Mimi nilikuwa nataka tu tight hug kwanza,nimfeel. Nikaamka na ile kiherehere ka nime-stretch arms ready for a hug. Msichana alinipita akisema “Raj mambo, nilikuwa nmekumiss” akaketi kwa kitanda bila hug. Hapo aliniembarazzz, roommates wakacheka, hadi ye pia akacheka. Hapo ndo nilitamani kuruka nje ya dirisha but sasa nikihepa, niachie nani hii mali !!

Tukapewa “free space” into some deep conversation…ata sikuwa attentive, kenye nilikuwa nataka tu ni “harvesting” macho ilikuwa imezubaa kwa cleavage. Yenye nilisikia ni “…I do love you, but on two conditions: Cut off your female friends and No sex until marriage…”
Sasa itakuwaje, na huku campus sex ni kama unit, alafu marriage tena, apo itakuwa ngumu. She was strict in every word she said and also tight as she was. Nikasema “okay babe, anything for you, but mwanzo I’ll think about your conditions.”

Nilirudi hostel, nikakusanya mbogii, kuwaambia venye nimeangukia fine ghel, nikaingia Instagram nikachomoa picha yake kuwaonyesha. Squad ika-approve ni mali legit. “ushafyeka?” kiswali kikaulizwa. Nikajibu “soon manduguu, soon, so far ni mamunju na ma-hug.” Deep down najua “kukula” ni tricky na hakuna kitu nilikuwa nmepewa ispokuwa maconditions.

After two days hivi nkamuita kwa room yangu sasa, nimpee majibu yake. Akasema atakuja 11:30am, skutaka hii time, nilitaka afternoon, ndo akuje ka amekula. Hiyo siku nili-mop, nika-spread vitanda zote. Nikaoga nikajispray ndo ninukie fiti. Nguo chafu nkapeleka room next. Mambo ikawa shwari. Pale na roommates tukaskia mtu anabisha. Nkasimama kuenda kufungua mlango, ready to receive my princess. Kwenda kufungua napata ni dem flani anatembezaga lollipops. “customer mtanun…” “si leo si leo” nilijibu haraka, alafu nkafunga mlango. Huyu hajui leo ndo ile siku, eeeish!
Kiasi kiasi mlango tena ikabishwa, this time alikuwa mamaa. Msupeng alikuwa amepiga luku moja waziiimu, mini-skirt ya grey, ina-reveal assets,top flani fiti afu viatu za bei, sijui ata zinaitwa aje. Nikajua leo its very possible. She was beautiful indeed. This time akanikujia na hug “heeey baabe” nkakumbuka mbogi waliniambia: A hug wothout ass grab is just a handshake. “Babe toa mkono kwa ass yangu” She was very strict bytheway,nikatii. Roommates ka kawa after salamu na introduction waka-left.

Sasa nikaanza kupambana hadi nichovye asali. “Stop it Raj, utaniharibia bra” “babe acha hizo, do it for me please” “babe I love you but I’m not ready for sex right now” “usikuwe hivo mamii, hii roho si yako”. Hizi ndo maneno zilikuwa zimejaza ile room. Sasa nikinyimwa nitasema nini kwa committee!! Aaaah! Tulisumbuana akakataa, vitu zingine si a must bytheway.
1p.m akasema anahisi njaa. “Babe twende tukule mess” ebu nisikie, nasema hivo ju pesa zote nilikuwa nimelipa pale mess, nilikuwa napiga order ka boss. Angekubali ninge-order alafu niseme:times two.
“Sijai na siezi kula mess, machakula zenye hazijaiva!” eeeeish! Sikieni huyu dem. Chakula me hukula niki-smile sahi analeta porojo kuihusu.

“Okay basii, twende tao” nasema hivo na nilikuwa na 200 Bob mbele nyuma, lakini mwanaume ni nani? Mwanaume ni mtu atajikaza kwa kila situation. Tukaishia tao, kwa hoteli alisuggest. Akaniuliza “Babe tukule nini?” nikajibu “anything you’ll order darling, anything for you” Wairimu akaitisha pilau na Delmonte mara mbili. Bill ilikuwa 900 Bob, nilikuwa na 200.

Nikajitoa kiasi nkamwambia naenda loo, kumbe nilikuwa naenda kuuliza mabeshte wanisaidie dooh, ju ilikuwa kiumane. Watatu walikuwa off, na mmoja hakushika simu. Sikuwa na option nkamtext budangu “Dad, kesho Friday kuna training ya Redcross, yafaa 1k for registration and training”

Nikarudi pale table. “is everything okay?” akauliza. “yes niko fiti sana” nikamjibu. Kidogo nikaona text message, ilikuwa ya TALA nilipe deni lao. Stress ilinitandika. All this time there was no conversation pale. Si heri ningeishia tu pale mess, Shetani ni mwongo kweeli. Kiasi tena naona message from new number “Bro niaje, niokolee ata 200,nmeuliza Dad anasema hadi Monday” That was my brother from highschool.

After half an hour tukamaliza kula. Nkasema “babe, mpesa yangu inahung sana.” Apa najua nilichoma, but hiyo ndo option nilikuwa nimebaki nayo.

She did not look surprised as I expected her to be. To her, everything was just okay.

Akatoa purse yake, noti za thao thao, akanipea thao nilipe ile bill.

Hii breed ni very rare. It’s the wish of every man to have a lady who would come in handy in time of difficulty, right? A lady who reciprocates everything in a relationship including financial support.

Tulizidi kuongea kwa simu. Siku moja akakuja pale room without notice. Apo sasa room ilikuwa messy, venye hukuwa kila siku. She held me tight, looked me right in the eyes. At that time I knew she was in love, as for me sikujua kama ni love ama lust.

Akasema “I’ve been thinking about us for a while, I’m ready to do anything for us darling.Kwanza funga mlango…promise you won’t say a word to anyone”
mmeskia hiyo kweeli?
Apo ndo ndume hujiona king.🤴🏾

0715820126
rajthemc55@gmail.com
FB:Mc Raj
Twitter/IG :@rajthemc

KEVOs. They never fail in their “chase”

Kuna huyu rafiki anaitwa Kevo, ali-spot mdem mfity niaje…Manzi alikuwa ameiva ile design yenye unateremsha barakoa😷kwanza ndo umcheki fity😅 yaani dem tu mfiine, chocolate color hivi [ata ka chocolate ni ya kulwa😂]. Huyo dem anaitwa Vee. Kumbuka short form ya Vee haijai na haiezi kuwa Vivian✋🏾😂😂 Ni Vanessa💯🔥 ka kawaida si mnajua kina Kevo hawalalishagi😂😂Alipewa namba na beshte ya Vee, kijana wetu akaslide kwa DM kama maganda😂😂

Kevo: Hi smart girl😍😍

Vee: Hi too.

Kevo: alaa😬na hii urembo yooote, haujui English!!! utafanya ata nikurudishie namba yako😉
Vee: We ni nani?

Kevo: chill, the response to “Hi” was never, is not and can never be “hi too”

Vee: (blueticks)

Kevo: ata unilishe blueticks bora umepata ujumbe😂

Vee: nmekuuliza we ni nani

Kevo: naitwa Kevo, lakini ntabambika sana nkiitwa Kevo wa Vee.

Vee: hehehe, umekuja sana msee😂😂 acha kunijazia dm, me sina sweets za kukupea✋🏾😂

Kevo: eeeeish, si we ni mfunny pia😂

Vee: where did you get my number?

Kevo: good question, ulipita pale base, na simu yangu me hueka phone location on, sa venye ulipita nka-scan available contacts, nikapata namba yako

Vee: 😂😂😂how can that even be possible, unanipima wewe.

Kevo: zii, siezi kudanganya. That’s how I got your number😆

Vee: apo umenibeba ndogo.Sa unataka nini?

Kevo: nakutaka wewe😍we hukua umenibamba.

Vee: aaawww🙈🙈
(Hapa Kevo akajua amepita semi-final😂 akiendelea vizuri atafika kwa penalty)

Kevo: yeah yeah mamii.

Vee: but I’m sorry,haiezi make, I have a boyfriend and I love him so much.

Kevo: sasa nani ameongelea relationship?

Vee: kwani what did you mean?

Kevo: I want you, I don’t want a relationship. Those are two different things.Sijui ka umenielewa apo🤔

Vee: sa mbona unagombana?

Kevo: sa unataka kulia?😂😂

(… blueticks…)

Kevo: sa mtu akisema ukweli analishwa blueticks, am I not supposed to express myself?

Vee: you are, just not in my dm❌

Kevo: aaaai, uskue rude hivo, hii roho si yako remboo.

Vee: 😂😂😂😂

(Kevo akacheki smati amerudi kwa moods poa)

Kevo: cheki venye nakubamba, ata kushinda your bf😆make the right decision baby girl.

Vee: ntakusema kwa manzi yako na atakuacha we Kevo, haiyaa😂

( wasomaji😂 mmeskia? Apa Kevo akajua it’s very very possbo. Kuingia tu chubwii🤣)

Kevo: me ata sina dem😉 najua unataka tu kujua ka nko na manzi.

Vee: hahaha, not really.

Kevo: unaskizaga gengetone?

(Kevo ni ka sa ameanza kukosa topic🚮😂 maybe ni strategy, who knows🤷🏾‍♂️)

Vee: definitely yes, I mean, who doesn’t like street music!

Kevo: eeeeey😘we sa tutablend vifity.

Vee: false hopes boychild✋🏾🤣

(…blueticks…)

(apa Kevo akanyamaza for more than 20 minutes, apa amenyamazishwa vibaya😂itabidi amechange strategy, ka sivyo, mali itamponyoka😂)

Vee: heeey stranger, what about street music?

( ata ka ni wewe si utajua dem ako interested na conversation, yaani unalisha dem blueticks na bado anatext💯😂 We ungeshinda apo na “how was your day” 😆)

Kevo: ooh,sorry,nilikuwa nakula supper😉

Vee: okay😂

Kevo: who’s your favorite genge artist?

Vee: I like Odi wa Murang’a, aaawww😍

Kevo: it’s him you want but it’s me you will get🤣

Vee: 🤣🤣🔥I give up🙌🏾

Kevo: don’t give up😂okay, aliimba;🎶sidai story nyingi me nadai kukukyamba, na ka ungekuwa tire singebakisha ata pienga…🎶

Vee: Jeeeez😆 I didn’t see that coming.

Kevo: so now you know😉

Vee: chill, aaah wait, tulia, what did you mean, you just wanna sleep with me☹️☹️

Kevo: I’m just being honest, is that a crime?

Vee: na ata huogopi kusema,ati honest☹️ jaribia kwingine nani.

Kevo: pole baas, ka unaona nmeongea vibaya, but me I just wanna be with you and make you happy.

Vee: ujue Kevo the last time nilidate nilipewa heartbreak mbaya sana, that’s why I don’t like entertaining random guys.

(ata amesahau alisema ako na chali😄)

Kevo: some guys are very wicked, how can someone break and leave such a pretty lady like you. Hell belongs to that nigga.

(weeeeeuh🔥🔥🤣🤣🤣)

Vee: it’s a very long story, I’m becoming emotional ata😢

Kevo: take it easy darling😘 what if we meet tomorrow, we talk in person, that would be appropriate.

(…blueticks…)

Kevo: heeey.

(chekini venye Kevo ana-force issues apa, anajua ashapewa penalty, bado tu kufungua bao😂)

Vee: heey, I’m here.

Kevo: what about my suggestion?

Vee: okay, but afternoon ndo ntakuwa free, but on one condition, in a public place.

Kevo: take it easy darling😘 what if we meet tomorrow, we talk in person, that would be appropriate.

(…blueticks…)

Kevo: heeey.

(chekini venye Kevo ana-force issues apa, anajua ashapewa penalty, bado tu kufungua bao😂)

Vee: heey, I’m here.

Kevo: what about my suggestion?

Vee: okay, but afternoon ndo ntakuwa free, but on one condition, in a public place.

Kevo: aaah, hiyo tu? tukutane tao, pale gardens.

Vee: that’s better.

Kevo: niice,sounds like a deal. Najua sahi uko emotional na staki kukusumbua, acha nkuallow upumzike.
(kijana plan inflow venye alitaka😂)

Vee: okay.

Kevo: have a Goodnight✨sweetheart😍😍

Vee: goodnight too. …
(Kevo still typing but he never sent the message: “si uongezee ata emojis sistee”) 😂😂

The following day walikutana. Apo ndo ile inaitwa “A shoulder to lean on” na ukumbuke ni ya Kevo🤣… after session Kevo alim-convince hadi wakaishia kejani… 😂hivo hivo tu akajishindia dem.

Moral: Go straight to the point, tell her what you want, akikubali sawa, asipokubali, pia sawa, jaribu next😂

For more stories, follow;

FB:Mc Raj
Twitter/IG: @rajthemc